RAIS MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA SIGARA
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli leo amezindua kiwanda cha kutengeneza
sigara cha Philips Morris International kilichopo mkoani Morogoro.
Rais Magufuli
ametembelea kiwanda hicho na kushuhudia namna sigara zinavyotengenezwa kuanzia
katika hatua ya kwanza mpaka sigara inapokamilika kwa matumizi au kwa ajili ya
kuuzwa.
Kwa upande wake Mmiliki
wa kiwanda hicho amesema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho kimeajiri zaidi ya watu
mia mbili na ishirini na nne ambao wanahusika katika kuhakikisha uzalishaji
unakwenda salama.
Hata hivyo,Rais Dkt.Magufuli
amempongeza mmiliki wa kiwanda hicho kwa kuzalisha ajira kwa wingi kwa
Watanzania.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments