MWENYEKITI WA BAJAJI MANISPAA YA MPANDA ANG’ATUKA


Mwenyekiti wa Chama cha madereva pikipiki za tairi tatu maarufu bajaji halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Rashid Rashid ametangaza kujiuzuru nafasi hiyo.
Katika taarifa yake ambayo ameitoa leo Bw.Rashid amesema, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja na kukosa ushirikiano kutoka kwa madereva wenzake,ukosefu wa ushirikiano kwa kamati yake na kutotekelezwa kwa mipango mbalimbali wanayoipanga kama chama.
Aidha amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni mgawanyiko wa wamiliki bajaji upande wa watumishi wa serikali kutozingatia kanuni na taratibu za umiliki wa chombo hicho cha usafiri.
Kwa upande wa wamiliki binafsi na madereva wao amesema wamekuwa wakikumbwa na mikasa ya kupelekwa kituo cha polisi pamoja na kulipishwa faini mara kwa mara bila utaratibu.
Hata hivyo Bw.Rashid amekanusha kula njama na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu Sumtra kuwatoza madereva bajaji mpaka kiasi cha shilingi 40,000 kwa ajili ya kujinufaisha.
Mapema mwaka huu,baadhi ya madereva bajaji walikuwa wakilalamika kutozwa fedha mpaka elfu arobaini ili kupewa namba ya usajili kwa ajili  katika maegesho wanayopangiwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA