RC KATAVI AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA KILIMO CHA PAMBA NA KOROSHO
Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amewataka wananchi kuchangamkia kulima kilimo cha korosho na pamba. Korosho Ametoa kauli hiyo wakati wa kukabidhi hundi kwa vikundi vya akina mama na vijana wasiriamali ambapo jumla ya milioni 37 zimetolewa kwa vikundi 12. Pamba Ameongeza kuwa upatikanaji wa mbegu za mazao hayo ni wa uhakika na tayari mkoa wa Katavi umepokea tani 51 za mbegu ya pamba kutoka bodi ya pamba Tanzania Huu ni mkakati wa Mkoa wa katavi kuondoa utegemezi wa zao la tumbaku ambalo limekumbwa na changamoto ya kukosekana wanunuzi . Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED