WAZIRI AVUNJA BODI
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe hii leo amevunja Bodi za Wakurugenzi za Majisafi na Usafi wa Mazingira za Jiji la Arusha na Musoma. Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari ambayo imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiy Prof.Kitila Mkumbo imeonesha Waziri Kamwelwe amesema kuwa amefanya hivyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa Bodi hizo. Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa tayari mchakato wa kuunda bodi mpya umeanza na zitatangazwa mara zitakapokamilika. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED