|
Mmoja wa wafanyabiashara akizungumza kueleza kero(PICHA NA.Issack Gerald) |
|
Wafanyaboiashara wakiwa wamkusanyika ndani na nje ya uzio wa studio za Mpanda Radio(PICHA NA.Issack Gerald) |
|
Baadhi ya wafanyabiasahara wakizungumza na Mpanda Radio na kueleza kero zao(PICHA NA.Issack Gerald) |
Mamia ya wafanyabiasahara wadogo wadogo katika Manispaa ya Mpanda
mkoani Katavi wameandamana mpaka katika kituo cha matangazo mpanda radio wakipinga
agizo la mkurugenzi wa Manispaa hiyo Michael Nzyugu kuyafunga masoko yasiyo rasmi.
Wakizungumza na Mpanda radio mapema leo wamesema, kitendo hicho hakikubaliki kwani mpaka sasa serikali
haijaandaa maeneo mbadala ya kufanyia biashara hizo.
Miongoni mwao wamesikika wakisema maeneo mengi wanayo takiwa kwenda
mara baada ya kuyahama maeneo yasiyo rasimi yanakabiliwa na miundombinu dhaifu
ikiwemo na mlundikano wa wajasiliamali.
Wiki iliyopita Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu
ameutangazia umma kuwa ifikapo tarehe 22 mwezi huu utakuwa mwisho wa masoko
bubu maarufu kama magenge.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments