WILAYA YA TANGANYIKA YAPIGA HATUA KIMAENDELEO KWA MIEZI 6
Na.Issack Gerald
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani
Katavi Salehe Muhando,amesema wilaya hiyo imepiga hatua za kimaendeleo katika
sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya,kilimo,umeme,Maji na miundombinu ya
barabara katika kipindi cha mwezi Julai mpaka Desemba 2017.
Muhando amebainisha hayo wakati
akiwasilisha taarifa ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo ikiwa
ni kutekelezwa kwa ilani ya chama cha Mapinduzi CCM katika kipindi cha mwezi Julai
mpaka Desemba mwaka jana.
Pamoja na mambo mengine amesema hatua
mbalimbali ya uchimbaji visima 21 vitakavyokamilika mwaka huu unaendelea kama
hatua ya kutatua tatizo la maji linalowakabili wananchi katika maeneo
mbalimbali ya vijiji vya wilaya hiyo.
Katika sekta ya nishati,Muhando
amesema Usambazaji wa umeme kwa vijiji vyote 43 vilivyoainishwa utaendelea huku
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya amesema,waanatarajia kufungua barabara
kutoka kiji cha St.Maria—Kabage,Vikonge—Bugwe,Isengure-Bujombe,Kona
Ikaka—Mnyagala na kutoka Mishambo kuelekea Ziwani Tanganyika.
Katika sekta ya Afya Muhando amesema,mpaka
kufikia mwezi Aprili Mwaka huu ujenzi wa kituo cha Afya Cha Mishambo kitakuwa
kimekamilishwa kuwa katika kiwango cha Hospitali huku juhudi nyingine kama hizo
zikielekezwa katika Kituo cha Afya Mwese.
Kwa mwaka wa fedha ujao wa 2018/2019
vituo vya afya vinatarajia kujengwa kijiji cha Kasekese kitakchohudumia pia
Sibwesa huku UJenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mnyagala na kituo cha afya
kitakachohudumia kata za kitakachohudumia kata za Ilangu na Ipwaga navyo
vikitarajiewa kujengwa kwa kasi ili kusogeza huduma kwa wananchi.
Aidha katika kuongeza ajira kwa
vijana,wanawake na Wakazi wa Tanganyika kwa ujumla,wilaya hiyo inatarajia
kujenga viwanda 7 vikiwemo viwanda vya kutengeneza chaki,kiwanda cha kufyatua tofali,kiwanda
cha kusindika alizeti,kiwanda cha kuzalisha sabuni na kiwanda cha kuzalisha
Blanketi na taulo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama
cha Mapinduzi CCM wilayani Tanganyika Bw.Yasini Mohamed Kibiriti pamoja na ambo
mengine amesisitiza viongozi wa chama na serikali kushirikiana kwa pamoja ikiwa
ni pamoja na kuandaa mpango kazi.
Utekelezwaji wa ilani ya Chama cha
Mapinduzi CCM ni matokeo ya kupata viongozi wa chama wanaoisimamia ilani na serikali
ambapo viongozi wa kichama katika Wilaya ya Tanganyika walipatiakana hivi
karibuni ambapo kwa upande wake Katibu wa CCM wilayani Tanganyika Warid Mngumi
ametoa pongezi kwa wote waliochaguliwa katika chaguzi zilizopita.
Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Hamad Mapengo,Makamu mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Bi.Theodora Romward Kisesa amesema baadhi ya changamoto
zilizoibuliwa na zilizokuwa zimeshaibuliwa zote wamezipokea tayari kwa kuanza
kuzifanyia kazi.
Kikao hicho maalumu ambacho
kimefanyika katika ukumbi wa chama cha Mapinduzi CCM wilayani
Mpanda,kimwashirikisha viongozi wa kichama na serikali wilaya ya Tanganyika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments