DC TANGANYIKA AONYA WATAKAOKIUKA TARATIBU ZA UCHAPAJI ALAMA ZA MIFUGO
Na.Issack Gerald
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani
Katavi Salehe Muhando amesema watakaokiuka zoezi la kutambua na kuweka alama ya
chapa katika mifugo atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria na taratibu za nchi.
Muhando ametoa kauli hiyo wakati
akiwasilisha taarifa ya utekelezaaji wa ilani ya chama cha Mpainduzi CCM katika
kipindi cha mwezi Julai mpaka Desemba 2017 kupitia kikoa maalumu cha chama
hicho ambacho kimefanyika Mjini Mpanda.
Aidha pamoja na mambo mengine amesema,katika
kipindi cha mwezi Julai mpaka kufikia Desemba mwaka jana,zaidi ya ng’ombe 158,114
wametambuliwa na kuwekewa alama ya utambuzi katika vijiji hamsini ambapo zoezi hilo
bado linaendelea katika vijiji vinne vilivyosalia Wilayani humo.
Katika hatua nyingine Muhando amesema
katika kipindi cha Julai mpaka Desemba Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
imekusanya zaidi ya shilingi milioni 22,590,400 kutokana na uvuvi haramu na shilingi
milioni 185,259,050 kutokana na ukamataji wa mazao ya misitu yaliyovunwa
kiholela ikiwa ni pamoja na magogo,mbao na mkaa huku suala la ufugaji nyuki
wilayani humo likiipatia mapato zaidi ya shilingi milioni mbili na wafugaji
wenyewe wa nyuki wakinufaika kwa kupata zaidi ya shilling milioni 500.
Awali kwa upande wa wajumbe wa kikao
hicho,wamesema utekelezwaji wa agizo hilo la seriikali kutambua na kupiga chapa
mifugo nchi nzima litapunguza uharibifu wa mazingira,kutokomeza wizi wa mifugo
na kutatua migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments