SHERIA MPYA VYAMA VYA SIASA YAUNDIWA KAMATI
Baraza la Vyama vya Siasa
limeunda kamati tano na kuzipa mwezi mmoja kupitia mapendekezo ya Sheria mpya
ya Vyama vya Siasa na Kanuni za usajili wa vyama.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Baraza hilo, John Shibuda alisema
kamati hizo zitafanya mapitio ya mapendekezo ya sheria mpya na kanuni ndani ya
wiki mbili ili kuona usahihi wa vifungu vilivyopo.
Alisema baada ya mapitio hayo kamati
hizo zinatakiwa zikamilishe maboresho ndani ya mwezi mmoja.
“Baraza limezipa wiki mbili kamati
ili ziweze kujipanga na kupitia mchakato halafu ndani ya mwezi mmoja waweze
kukamilisha na kutoa taarifa za kutosha,” alisema Shibuda.
Alisema baada ya maboresho
kukamilishwa watatoa mapendekezo kwa mwenyekiti ambaye ataitisha kikao na
kuyajadili kisha itaandaliwa rasimu.
Shibuda alisema, hadi sasa mchakato
wa kutunga sheria na kanuni za usajili wa vyama vya siasa bado haujatekelezwa
na badala yake zimeunda kamati ambazo zitachakata mapendekezo.
Alisema baraza ndilo litakaloridhia
yapi yanafaa kuwa mapendekezo ya vyama vya siasa kwa ajili ya kutungwa kwa
sheria.
Shibuda alisema baraza hilo lipo
huru na vyama vyote vimeshiriki wakiwamo wajumbe kutoka Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa),ambao wamewakilishwa na Salum Mwalimu ambaye ni Naibu Katibu
Mkuu Zanzibar (Chadema) na wajumbe wengine kutoka vyama mbalimbali.
Amezitaja kamati zilizoteuliwa na
viongozi wake ni Kamati ya Bunge na Siasa, Mwenyekiti Juju Martini Danda
(NCCR-Mageuzi) na Makamu Mwenyekiti ni Mohamed Masoud Rashid (Chauma).
Nyingine ni kamati ya Sheria na
Utawala Bora ambapo mwenyekiti wake ni Hassan Almas (NRA) na Makamu wake ni
Said Sudi.
Shibuda aliitaja pia Kamati ya
Maadili na Mahusiano inayoongozwa na Mohamed Ally Abdallah (Demokrasia Makini)
na Peter Magwira (Democratic Party).
Kamati ya fedha Mwenyekiti John
Cheyo (UDP) na Salum Mwalimu ambapo ile ya Uongozi wa Baraza la vyama vya
Siasa, Shibuda na Dk. Abdallah Juma Saadala.
Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For
Democratic Change (ADC), Doyo Hassan alisema hajaona sababu za
mapendekezo hayo kuundiwa kamati.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments