WABUNGE 11 WAVULIWA UANACHAMA
Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe jana kimetangaza kuwafukuza wabunge wake 11 ambao ni washirika wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe.
Maamuzi
ya kuvuliwa uanachama wabunge hao yalitolewa na kutangazwa Bungeni na Naibu
Spika wa Bunge la Zimbabwe,Mabel Chinomona baada ya Bunge hilo kupokea barau
kutoka kwenye chama cha ZANU PF iliyosema wabunge hao wamefukuzwa kwa mujibu wa
Katiba ya Zimbabwe kupitia kifungu namba 129 (1) (k).
Naibu Spika alisema kuwa wabunge
waliofukuzwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani, aliyekuwa Waziri
wa Nishati,aliyekuwa Waziri wa Michezo, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na
wabunge wengine wa majimbo mbalimbali nchini humo.
Kufuatia zoezi hilo Bunge
limetangaza nafasi wazi katika majimbo hayo 11 na kuijulisha Tume ya Uchaguzi
ya Zimbabwe kuhusu uwepo wa nafasi za wazi katika majimbo hayo kwa mujibu wa
Katiba ya nchi hiyo ili zoezi la uchaguzi liweze kufanyika kupata wawakilishi
wa Wanachi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments