MKOANI WA RUKWA WAZINDUA KAMPENI YA UPANDANI MITI
MKOA wa Rukwa umezindua kampeni ya upandaji miche ya
miti kwa lengo la kuhifadhi mazingira ambapo katika kipindi cha mwaka huu
unatarajia kupanda jumla ya miche milioni sita katika halmashauri
zote nne za mkoa huo.
Akizundua kampeni katika halmashauri ya wilaya ya Kalambo katika
mji wa Matai,mkuu wa mkoa huo Joachim Wamgabo alisema kila halmashauri
italazimika kupanda miche isiyopungua milioni 1.5 ambapo mpaka sasa tayari mkoa
mzima umeotesha miche milioni 2,173,649 sawa na asilimia 36 ya miche itakayo
pandwa.
Alisema yeye amezindua kampeni hiyo kinachofuata ni
watendaji wa serikali kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza na ambapo itakapofikia
mwishoni mwa mwaka halmashauri ambayo haitafikia lengo itatozwa faini ya
shilingi milioni moja na fedha hizo itakabidhiwa halmashauri ambayo imetekeleza
kampeni hiyo kwa asilimia mia moja.
Awali kabla ya kuzindua kampeni hiyo Wangabo alimuagiza
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo Simon Ngagani amwajibishe Afisa
mtendaji wa kiji cha Matai Ester Mwashambwa kwa kitendo cha kushindwa
kuwahamasisha wananchi wajitokeze katika uzinduzi wa kampeni hiyo kwani
waliofika walikuwa ni wanafunzi wa shule ya sekondari Matai na watumishi wa
serikali.
Alisema wananchi ni wadau wakubwa katika suala la uhifadhi
mazingira na ndiyo wakataji miti wakubwa kwa lengo la kupata nishati ya mkaa na
kuni lakini kitu cha ajabu hawakuwepo katika uzinduzi huo hali iliyomkera mkuu
huyo wa mkoa.
Naye mwakilishi wa wakala wa misitu Tanzania TFS wilayani Kalambo
Herman Ndanzi alisema wakala huo una jumla ya hekta 1192 ambazo unazihudumia
licha ya kuwa bado jitihada zinafanyika za kupanda miti ili kuongeza misitu.
Alisema wakala huo umewapatia wananchi kilogramu 6 za mbegu za
miti ya aina tofauti ili wakaipande ambapo itasaidia kuhifadhi mazingira na
kuwa inaendelea na suala kuwaelimisha wananchi waache kuharibu misitu.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments