WAKAZI WILAYANI MPANDA WALALAMIKIA UBOVU WA MIUNDOMBINU YA RELI
Wananchi wilayani Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia shirika la reli kwa kutorekebisha miundombinu ya reli kwa wakati katika eneo la Ugala mpaka Rumbe.
Wananchi hao wameeleza
kuwa kumekua na ajali nyingi zikitokea kutokana na miundombinu ya eneo hilo
kutokuwa salama kwa usafiri hali inayosababisha kupotea kwa mizigo.
Mkuu wa kituo cha
reli Mpanda Bw.Vivian Lyapembile amesema kuwa pamoja na
changamoto wanazopata kwa sasa ila wana ufahamu na tatizo hilo na tayari wameanza mchakato wa kukarabati
eneo hilo.
Hivi karibuni kumekuwa na
changamoto ya usafiri kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa treni hali
inayosababishwa uchakavu wa miundo mbinu kwa baadhi ya maeneo pamoja na maeneo
mengine reli kusombwa maji ya mvua zinazoendelea kunyesha.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments