MSIMAMO MPYA WA RAIS MSEVENI KUHUSU KUNYONGA WATU
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anatafakari uwezekano wa kuanza tena kuwanyonga wahalifu nchini humo.
Rais
Museveni amesema licha ya kwamba yeye ni "Mkristo" kuwa dini yake
imemzuia kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya wale ambao wamehukumiwa kunyongwa,
hata hivyo amesema hali hiyo imekuwa ikiwatia moyo wahalifu.
Kiongozi huyo ametoa kauli
hiyo wakati wa sherehe za kuhitimu kwa askari wa idara ya magereza katika
gereza la Luzira jijini Kampala.
Mpaka
sasa ni miaka 13 sasa tangu Uganda ilipotekeleza hukumu ya kifo dhidi ya
wahalifu.
Watetezi
wa haki za kibinadamu wameshutumu tamko hilo la Rais Museveni na kusema adhabu
ya kifo haikomeshi uhalifu.
Mara ya mwisho kwa Rais
Museveni kuidhinisha hukumu ya kifo itekelezwe ilikuwa katika gereza la Luzira
mwaka 1999 na mwaka 2005 aliidhinisha mahakama ya kijeshi kutekeleza hukumu ya
kifo
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments