CHADEMA WATEUA WAGOMBEA MAJIMBO YA SIHA NA KINONDONI
Kamati
Kuu ya Chama imemaliza Vikao vyake Leo Januari 19 imefanya uamuzi wa kushiriki
kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa
kufanyika Februari 19 mwaka huu.
Baada
ya uamuzi huu kufanyika,Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo ambapo
Mhe.Salum Mwalim Juma ameteuliwa kugombea jimbo la Kinondoni huku Bw. Elvis
Christopher Mosi akiteuliwa kugombe jimbo la Siha.
Kwa mjibu wa John Mrema ambaye ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika.
Kwa mjibu wa John Mrema ambaye ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika.
Wagombea
hao wanatajia kurejesha fomu hizo kesho jumamosi kwa ajili ya uteuzi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments