SERIKALI YATOA TAHADHARI KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA CHIKUNGUNYA
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa homa ya
Chikugunya ambao umeripotiwa na vyombo vya habari kutokea jijini Mombasa nchini
Kenya.
Mh.Dk.Ummy Mwalimu-Waziri wa Afya |
Kwa
mujibu wa Wizara ya Afya ugonjwa wa Chikunganya unasababishwa na kirusi ambacho
kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes.
Taarifa
ya wizara hiyo inaeleza kuwa ugonjwa huu si mgeni nchini Tanzania kwani
ulishawahi kutokea.
Dalili
za ugonjwa wa Chikungunya ni homa kali,kuumwa kichwa,maumivu ya
viungo,uchovu,kichefuchefu,kizunguzungu na wakati mwingine tumbo kuuma
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments