WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA WAKITUHUMIWA WIZI WA FEDHA KWA KUTUMIA SIMU
Na.Issack Gerald-Mpanda Watu wawili wakazi wa kijiji cha Ikaka kata ya Mnyagala wilayani Mpanda mkoani Katavi,wamefikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda wakikabiliwa na shtaka la wizi wa fedha kwa njia ya simu ambayo ni mali ya Charles Lubasha mkazi wa Kakese.