WAKUU WAPYA WA MIKOA WAAPISHWA,HOTUBA YA RAIS MAGUFULI KITANZI KWAO
Na.Issack Gerald
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametoa siku kumi na tano kwa Wakurugenzi wa
halamshauri zote nchini Kufuta Majina ya Wafanyakazi hewa wanaolipwa Mishaha.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo
wakati akiwaapisha wakuu wa Mikoa Wapya 26 wa Tanzania bara aliowateua siku ya
jumapili.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli
amewataka wakuu wa Mikoa hao Kuhakikisha wanalinda Usalama wa Mipaka ya nchi na
Kuhakikisha kila Mtanzania anafanya kazi huku akiagiza Kukamatwa kwa Vijana
wanaocheza Michezo ya pulu wakati wa Kazi badala ya Kufanya kazi.
Miongoni mwa wakuu wa Mikoa
walioapishwa mbele leo ni Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga anayechukua nafasi ya
Dr Ibrahim Msengi.
Rais Magufuli akifafanua sababu za
kuweka wakuu wa mikoa wanajeshi katika mikoa ya Rukwa,Katavi,Kigoma na Kagera
amesema kuwa ni mkakati wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwepo
zaidi ikizingatiwa kuwa ni mikoa iliyopo mpakani mwa nchi jirani.
Comments