Posts

Showing posts from November 13, 2017

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI IMEWATAKA WAVUVI WAKACHUKUE INJINI BOTI WAVUE SAMAKI KWA TIJA

Image
Na.Issack Gerald SERIKALI imetoa wito kwa wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania waliopo mwambao wa bahari na maziwa kuhamasisha vikundi vya wavuvi waliopo katika maeneo yao kupitia Halmashauri zao kujitokeza na kuchukua ruzuku ya boti injini 24 zilizobaki kwa ajili ya kuendesha shughuli za uvuvi zenye tija. Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mh. Abdallah Hamis Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Vijijini Mh.Moshi Suleiman Kakoso aliyetakakujua  ni lini serkal;I itawapatia vitendea kazi wavuvi wadogowadogo. Pamoja na mambo mengine Mh. Abdallah Hamis Ulega akijibu swali hilo amesema kwa mwaka wa fedha Mwaka wa fedha 2015/2016 serikali ya awamu ya tano ilitenga shilingi 400 zilizonunua boti injini 73 ambapo kati ya hizo injini 49 zilishachujkuliwa na vikundi vya uvuvi  nchini kwa mtindo wa ruzuku kupitia Halmashauri zao ambapo serikali inachangia 40 na vikundi 60%. Naye Mbunge viti maalumu Mkoani Katavi Anna Lup...

KWA MARA YA KWANZA HAPA NCHINI SIMBA ATIBIWA KWA KUFANYIWA UPASUAJI

Image
  Na Geofrey Stephen Ngoro Ngoro Taasisi ya wanyama pori TAWRI kupitia mtaalam wake wa wanyama pori Dkt.Ernest Mjingo amefanikiwa kuokoa maisha ya simba wenye matatizo ya ugonjwa ngiri kwa simba huyo mtoto. Simba Dkt.Ernest Mjingo amesema kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji na kufanikiwa kwa asilimia mia moja na kwamba simba huyo ataishi bila maradhi mara baada ya kupona na kurudi katika hali yake ya mwanzo. Hii ni mara ya kwanza kwa simba hapa nchini kufanyiwa upasuaji na kuimarika tofauti na wanyama wengine kupata maradhi na kufa kwa kukosa matibabu ya kitaaluma Msemaji wa wa ifadhi ya mamlaka ya ngoro ngoro worlter mairo amesema wanashukuru kuona simba huyo kupata matibabu na badae kuendelea kutangaza utalii wa ndani kwa kuongeza pato la taifa kupitia secta ya utalii Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

ASKARI WA WANYAMA PORI MKOANI ARUSHA WAMEINGIA MGOGORO NA WAFUGAJI

Image
Na Geofrey Stephen-Arusha. Wakazi wa kata za Ololosokwan,Soitsambu wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,wamewashutumu baadhi ya askari wa mamlaka ya hifadhi ya Serengeti(Senapa) kukamata mifugo yao katika ardhi za vijiji na kisha kuipeleka ndani ya hifadhi. Moja ya alama inayotambulisha Mkoa wa Arusha Mwenyekiti wa kijiji cha Kirtalo,Yohana Toroge amesema,jumla ya ng’ombe wake 1000 walikamatwa   Novemba 4 mwaka huu  wakati wakielekea kunywa maji kisimamani na kisha kupelekwa ndani ya maeneo ya hifadhi. Aidha Wakazi hao walitoa kilio chao mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Olosokwan uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimila. Mkuu wa mamlaka ya hifadhi ya Serengeti (Senapa), William Mwakilema alijibu shutuma hizo na kusema wakazi hao wanatunga uongo kwa kuwa hakuna askari wake  anayekamata mifugo ndani ya ardhi za vijiji na kuwalipisha faini kubwa. Wenyekiti wa halmashauri ya Ngorongo...

SHIRIKA LA WORLD VISION KUKABIDHI VIFAA TIBA KWA VITUO VYA AFYA 111 MKOANI

Image
Na.Isaac Isaac-Kigoma Jumla ya vituo vya afya 111 vintarajiwa kunufaika kwa kupatiwa vifaa tiba pamoja na ujenzi wa wodi na vyumba vya upasuaji katika wilaya tatu (3) za mkoa wa Kigoma. Kigoma Ujiji Hatua hiyo ni kupitia mradi wa uboreshaji wa huduma ya mama na mtoto unaofadhiliwa na shirika la World Vision lengo likiwa ni kutoa hamasa kwa wajawazito  kujifungulia katika vituo vya afya. Kauli hiyo imetolewa na meneja mradi Monica Dedu kutoka katika shirika la world Vision wakati wa semina elekezi kwa viongozi wa madhehebu ya kidini pamoja na madiwani  katika Manispaa ya Kigoma ujiji ili kutia moyo na kuhamasisha  jamii kuona umuhimu wa kutumia huduma za afya. Naye Mganga mkuu wa mkoa Kigoma Poul Chaote amesema asilimia 65 ya akina mama wajawazito ndio wanaofika katika vituo vya afya kwa ajili ya kujifungua huku wengine wakijifungulia majumbani jambo linalohatarisha afya zao lakini pia usalam wa maisha ya watoto Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa kidini w...

MBUNGE KAPUFI WA MPANDA AUNGURUMA BUNGENI TOZO ZA ZIMAMOTO

Image
Na.Issack Gerald Serikali  imesema tozo inayotozwa na jeshi la zima moto na uokoaji kwa lengo la kutoa kibali cha ujenzi ni kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2015. Katika picha Mh.Sebastian Kapufi anayesalimiana na waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ufafanuzi huo umetolewa leo na Naibu waziri wa Wizara ya mambo ya ndani ya nchi  ambapo amesema awali sheria hiyo ilikuwa haifuatwi ila kwa sasa utekelezaji umeanza na hivyo kila mwananchi anatakiwa kutii sheria hiyo. Kauli ya Waziri Naibu Waziri-Mhandisi Hamad Yusuf Masauni wakati Akijibu swali la mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastiani Simoni Kapufi aliyetaka kujua  kama tozo hizo zipo kihalali. Aidha naibu waziri amesema ili kuondokana na majanga yanayotokana na ujenzi holela lazima wananchi walipie tozo hiyo ili wapate kibali cha ujenzi. Wiki iliyopita,Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Katavi wiki lilitangaza kushuka kwa bei ya tozo hiyo kutoka shilingi 150,000/=na kufikia 50,000/= ili kila wananchi amudu gharama...

BAADA YA HUKUMU YA LULU,MAMA WA MAREHEMU KANUMBA AZUNGUMZA

Image
Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema leo atakwenda makaburi ya kinondoni alipoziikwa mwanaye ili kumzika upya. Mama wa Marehemu Kanumba Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo. "Kwa sasa sina la kusema ila  naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba" . Mama Kanumba Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake. Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMI...

CWT MKOANI RUKWA:WALIMU TIMIZENI WAJIBU WENU KABLA YA KUDAI HAKI

Image
KIMCHAMA cha walimu CWT wilayani Kalambo mkoani Rukwa kimewataka walimu kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kabla ya kudai haki mbalimbali ikiwemo nyongeza ya mshahara. Ushauri huo umetolewa na katibu wa chama hicho Peter Simwanza wakati wa sherehe maalumu za kuwapongeza walimu wa shule za msingi zilizopo katika kata ya Ulumi ambao wanafunzi wao walifaulu vizuri kwa kupata kiwango cha alama A katika masomo ya kuhitimu darasa la saba pamoja na shule zilizofanya vizuri. Alisema baadhi ya walimu wamekuwa mbele katika kudai haki zao mbalimbali ikiwemo nyongeza ya mshahara lakini hawatimizi wajibu wao kwamujibu wa sheria.  Simwanza alisema walimu wilayani humo wanapaswa kutekeleza sheria zote za kazi kwa mujibu wa mkataba wa ajira ndipo wadai haki zao kwa mwajiri.  Katika hatua nyingine,aliwataka walimu kutokuwa wanyonge wanapoona haki zao zimekiukwa kwa kuwa maslahi yao yapo mikononi mwao lakini kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu.  Naye Sabina Mwamwezi mwakilishi...

KIJANA AMEUAWA AKIIBA MIHOGO MKOANI RUKWA

Image
KIJANA aliyetambulika kwa jina la zakaria Katembo (30) mkazi wa kijiji cha Kakoma Kata ya Kipundu  wilayani Nkasi mkoani Rukwa,ameuawa kwa kupigwa mpini na watu wasiojulika na wanaodaiwa kuwa na hasira kali. Mwenyekiti wa kijiji cha Kakoma  Patrick Mwami alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4 za usiku baada ya wananchi wa kijiji hicho wanaodaiwa kuwa na hasira Kali kumvamia kijana huyo akiwa shambani alikokuwa akichimba mihogo na kumuua kwa kipigo. Alisema wananchi baada ya kufanya mauaji hayo waliuacha mwili wa marehemu huyo katika shamba hilo na kuondoka na hawakubainika ni wakina nani waliofanya tukio hilo. Kwa upande wake diwani wa kata ya Kipundu John Kapandila amesema  baada ya tukio hilo aliutaka uongozi wa kijiji kutoa taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe. Aidha aliitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi badala yake wafuate sheria ili iweze kuchukua mkondo wake katika kuwaadhibu wahalifu. Kwau pand...

SERIKALI IMEANIKA SABABU ZA KUJITOA OGP,ATISHIA KUFUTA BARAZA LA MADIWANI KIGOMA MJINI

Image
Serikali imekiri kujitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), ambao serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiunga Septemba 21 mwaka 2011.        Mh.George Mkuchika Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora,Mh.George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe lililohoji kwanini serikali imejitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji serikali kwa uwazi (OGP). Mh.Mkuchika amesema baada ya serikali kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa ambapo ameongeza kuwa sio nchi ya kwanza kujitoa kwenye mpango huo. Kwa upande mwingine Mh.Zitto ameshauri kuwa serikali ingeendelea kuwa mwanachama wa (OGP) ingefaidika kwa sulaa la ndege za Bombadier ambazo zimekwama nchini Canada kutoka na nchi hiyo kuwa ndiyo mwenyekiti wa sasa wa OGP. Hata hivyo Waziri amesisitiza mahusiano ya Tanzania na Canada ni mazuri bila...

LULU AHUKUMIWA JELA MIAKA 2 KWA KESI YA KUUA

Image
Na.Issack Gerald Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia. Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo na kusema mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira,hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela. Baada ya hapo jaji rumanyika aliwapa nafasi upande wa mshtakiwa kujitetea ambapo wakili wake Peter Kibatala alimtetea mshakiwa kwa kusema mshtakiwa anategemewa na familia yake. Mara baada ya utetezi huo, Jaji Rumanyika alitoa hukumu yake na kumuamuru mshtakiwa kwenda jela kwa miaka miwili. Elizabeth Michael (Lulu) anahukumiwa kwa kumuaa aliyekuwa mpenzi wake Steven Charles Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake,mnamo April 7, 2012. Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

MIMBA KWA WANAFUNZI KAA LA MOTO KWA WAZAZI NA WANAFUNZI MKOANI RUKWA

Image
Na.Issack Gerald Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa shule mkoani humo kumkamata na kuwaweka ndani Mzazi na Mwanafunzi yeyote wa kike atakayebainika kuwa na mimba hadi hapo watakapomtaja anaehusika na mimba hiyo. Amesema kumekuwa na tabia ya kumalizana kienyeji huko majumbani na matokeo yake Watuhumiwa hawafikishwi sehemu husika ili waweze kuwajibishwa. Ametoa agizo hilo baada ya kusomewa taarifa ya Shule ya sekondari Kilando iliyopo Wilayani Nkasi wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa maabara pamoja na kuongea na Wanafunzi, na kupewa taarifa ya mimba saba kwa kipindi cha January hadi October mwaka huu wa 2017 huku kesi zote zikiwa zimefikishwa polisi. Alitahadharisha kuwa shule yoyote atakayoitembelea katika ziara yake hiyo ya kujitambulisha katika Halmashauri nne za mkoa huo,ihakikishe inabainisha hatua zilizochukuliwa kwa Watuhumiwa na zilipofikia na si kueleza tu idadi ya kesi na kuwepo kwa kesi hizo polisi. Kwa upande ...