WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI IMEWATAKA WAVUVI WAKACHUKUE INJINI BOTI WAVUE SAMAKI KWA TIJA
Na.Issack Gerald
SERIKALI imetoa wito kwa wabunge wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania waliopo mwambao wa bahari na maziwa kuhamasisha vikundi
vya wavuvi waliopo katika maeneo yao kupitia Halmashauri zao kujitokeza na
kuchukua ruzuku ya boti injini 24 zilizobaki kwa ajili ya kuendesha shughuli za
uvuvi zenye tija.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni
Dodoma na naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mh.Abdallah Hamis Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa
Mpanda Vijijini Mh.Moshi Suleiman Kakoso aliyetakakujua ni lini serkal;I itawapatia vitendea kazi
wavuvi wadogowadogo.
Pamoja na mambo mengine Mh. Abdallah Hamis Ulega akijibu swali hilo amesema kwa mwaka
wa fedha Mwaka wa fedha 2015/2016 serikali ya awamu ya tano ilitenga shilingi 400
zilizonunua boti injini 73 ambapo kati ya hizo injini 49 zilishachujkuliwa na
vikundi vya uvuvi nchini kwa mtindo wa
ruzuku kupitia Halmashauri zao ambapo serikali inachangia 40 na vikundi 60%.
Naye Mbunge viti maalumu Mkoani
Katavi Anna Lupembe amemwomba wizara
kufika katika maeneo ya Ikola,Karema,Kapalamsenga
na maeneo mengine yanayoendesha shghuli za uvuvi ili kusikiliza keromzao suala
ambalo waziri Abdallah Hamis Ulega amemjibu kuwa baada ya kikao cha
tisa wafika ziwani Tanganyika ili kusikiliza kero ili zitatuliwe.
Kwa upande wake Zainabu Katimba
Mbunge viti maalumu Mkoani Kigoma baada
ya kuuliza swali akitaka kutambua hatua zinazofanywa
na serikali kuhakkikisha wavuvi wanazifikia fursa mbalimbali,waziri Abdallah Hamis Ulega amesema kwa mwaka wa fedha 2017/2018
serikali imekwishatenga shilingi milioni 100 ili kuendelea kusaidia vikundi vya
uvuvi vitakavyokuwa vimeundwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments