MBUNGE KAPUFI WA MPANDA AUNGURUMA BUNGENI TOZO ZA ZIMAMOTO
Na.Issack
Gerald
Serikali imesema tozo inayotozwa na jeshi la zima moto
na uokoaji kwa lengo la kutoa kibali cha ujenzi ni kwa mujibu wa sheria ya
mwaka 2015.
Katika picha Mh.Sebastian Kapufi anayesalimiana na waziri Mkuu Kassim Majaliwa |
Ufafanuzi huo umetolewa leo na Naibu waziri wa Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ambapo amesema awali sheria hiyo ilikuwa
haifuatwi ila kwa sasa utekelezaji umeanza na hivyo kila mwananchi anatakiwa
kutii sheria hiyo.
Kauli
ya Waziri Naibu
Waziri-Mhandisi Hamad Yusuf Masauni wakati Akijibu swali la
mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastiani Simoni Kapufi aliyetaka kujua kama tozo hizo zipo kihalali.
Aidha naibu waziri
amesema ili kuondokana na majanga yanayotokana na ujenzi holela lazima wananchi
walipie tozo hiyo ili wapate kibali cha ujenzi.
Wiki iliyopita,Jeshi la
zimamoto na uokoaji mkoani Katavi wiki lilitangaza kushuka kwa bei ya tozo hiyo
kutoka shilingi 150,000/=na kufikia 50,000/= ili kila wananchi amudu gharama.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments