ASKARI WA WANYAMA PORI MKOANI ARUSHA WAMEINGIA MGOGORO NA WAFUGAJI
Na Geofrey Stephen-Arusha.
Wakazi wa kata za Ololosokwan,Soitsambu
wilayani Ngorongoro mkoani Arusha,wamewashutumu baadhi ya askari wa mamlaka ya
hifadhi ya Serengeti(Senapa) kukamata mifugo yao katika ardhi za vijiji na
kisha kuipeleka ndani ya hifadhi.
Moja ya alama inayotambulisha Mkoa wa Arusha |
Aidha Wakazi hao walitoa kilio chao mbele ya
waandishi wa habari katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la
Olosokwan uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimila.
Mkuu wa mamlaka ya hifadhi ya Serengeti
(Senapa), William Mwakilema alijibu shutuma hizo na kusema wakazi hao wanatunga
uongo kwa kuwa hakuna askari wake anayekamata mifugo ndani ya ardhi
za vijiji na kuwalipisha faini kubwa.
Wenyekiti wa halmashauri ya Ngorongoro,Mathew
Siloma amesema wao kama halmashauri wanapinga vikali vitendo vya baadhi ya
askari wa Senapa kukamata mifugo ndani ya makazi ya watu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments