MIMBA KWA WANAFUNZI KAA LA MOTO KWA WAZAZI NA WANAFUNZI MKOANI RUKWA
Na.Issack
Gerald
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa shule mkoani
humo kumkamata na kuwaweka ndani Mzazi na Mwanafunzi yeyote wa kike
atakayebainika kuwa na mimba hadi hapo watakapomtaja anaehusika na mimba
hiyo.
Amesema kumekuwa na tabia ya kumalizana kienyeji huko majumbani na
matokeo yake Watuhumiwa hawafikishwi sehemu husika ili waweze kuwajibishwa.
Ametoa agizo hilo baada ya kusomewa taarifa ya Shule ya sekondari
Kilando iliyopo Wilayani Nkasi wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa maabara
pamoja na kuongea na Wanafunzi, na kupewa taarifa ya mimba saba kwa
kipindi cha January hadi October mwaka huu wa 2017 huku kesi zote zikiwa
zimefikishwa polisi.
Alitahadharisha kuwa shule yoyote atakayoitembelea katika ziara
yake hiyo ya kujitambulisha katika Halmashauri nne za mkoa huo,ihakikishe
inabainisha hatua zilizochukuliwa kwa Watuhumiwa na zilipofikia na si kueleza
tu idadi ya kesi na kuwepo kwa kesi hizo polisi.
Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilando Erneo
Mgina amesema kati ya Wanafunzi saba waliopata ujauzito Wanafunzi watatu ni wa “A
– Level” na wanne ni wa “O – Level” na kueleza kuwa wengi wao hupata mimba
wakati wa likizo na huwabaini pale tu wanaporudi shule na kuwapima.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments