KIJANA AMEUAWA AKIIBA MIHOGO MKOANI RUKWA
KIJANA aliyetambulika kwa jina la zakaria Katembo
(30) mkazi wa kijiji cha Kakoma Kata ya Kipundu wilayani Nkasi
mkoani Rukwa,ameuawa kwa kupigwa mpini na watu wasiojulika na wanaodaiwa kuwa
na hasira kali.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kakoma Patrick
Mwami alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4 za usiku baada ya
wananchi wa kijiji hicho wanaodaiwa kuwa na hasira Kali kumvamia kijana huyo
akiwa shambani alikokuwa akichimba mihogo na kumuua kwa kipigo.
Alisema wananchi baada ya kufanya mauaji hayo
waliuacha mwili wa marehemu huyo katika shamba hilo na kuondoka na
hawakubainika ni wakina nani waliofanya tukio hilo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kipundu
John Kapandila amesema baada ya tukio hilo aliutaka uongozi wa kijiji
kutoa taarifa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Aidha aliitaka jamii kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mikononi badala yake wafuate sheria ili iweze kuchukua
mkondo wake katika kuwaadhibu wahalifu.
Kwau pande wake mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilayani Nkasi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said
mtanda alisema watawasaka wote waliofanya mauaji hayo na kuwabaini ili sheria
ichukue mkondo wake.
Naye Kamanda wa Polisi mkoani humo George
Kyando alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi wanaendelea na
uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa wa mauaji hayo ili wafikishwe kizimbani
wakajibu tuhuma zitakazo wakabili.
Hata hivyo alionya tabia ya baadhi ya
wananchi kujichukulia sheria mikononi kwani kufanya hivyo ni makosa na lazima
wanaofanya hivyo wachukuliwe hatua kali ili kukomesha mauaji holela.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments