VIONGOZI WENGINE WALIOWAHI KUAPISHWA NA KUJITANGAZA KUWA MARAIS KAMA ODINGA BARANI AFRIKA
Kiongozi
wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga Jumanne aliapishwa kuwa 'rais wa
wananchi' nchini humo baada ya kusema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta
katika uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo Oktoba mwaka jana.
Mgombea
mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper hakujitokeza kwa sherehe hiyo ya
kuapishwa, ingawa alikuwa miongoni mwa waliotarajiwa kuapishwa.
Bw
Odinga alisema Bw Musyoka, ataapishwa "baadaye".
Waziri
mkuu huyo wa zamani hayuko peke yake katika kujaribu kujitangaza marais, kukiwa
bado kuna rais mwingine madarakani.
Raila Odinga Akiapa |
Wengine ni akina nani?
Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi, Nigeria Moshod Abiola, Uganda Kiza
Besigye na Jean Ping wa Gabon ni miongoni mwa viongozi wa upinzani wa Afrika
ambao wamejaribu kujitangaza kuwa marais, na sasa Raila Odinga amejiunga na
orodha hii.
Etienne Tshisekedi
Kufanana
kati ya Tshisekedi na Odinga ni kwamba wote wawili walikuwa kizuizini bila
kufunguliwa mashtaka, wote walihudumu kama mawaziri wakuu na wote waligomea
uchaguzi wa urais; Tshisekedi mwaka 2006, Odinga katika 2017.
Mwezi
Novemba 2011,Tshisekedi alijitosa kwenye kinyang'anyiro dhidi ya mtoto wa
Laurent Kabila, kisha aliamua kujiandalia kiapo mwenyewe na kuapishwa nyumbani
kwake na mkuu wa watumishi wake Albert Moleka baada ya jaribio la kujiapisha
katika uwanja wa Wahanga, Kinshasa kutibuka. Baadaye, aliwekwa katika kizuizi
cha nyumbani.
Moshood Abiola
Moshood Abiola |
Nigeria,Moshood
Abiola alijitangaza mwenyewe kuwa rais kipindi ambacho Rais Sani Abacha
alipokuwa madarakani.
Hii
ni baada ya kutembelea nchi nyingi za Magharibi,kutafuta msaada ili kumkabili
Abacha katika utawala wake.
Alikamatwa
na kushtakiwa kwa uhaini na kufungwa jela kwa miaka minne hadi ilipofika mwaka
1995,Siku aliyoachiwa kutoka gerezani, alikutana na ujumbe wa Marekani na
kuhuduria mkutano.
Baada
ya kupewa chai akiwa mkutanoni alianguka na kuzimia na hatimaye kufariki dunia.
Jean Ping
Mwaka
2016 Gabon, kiongozi wa upinzani Jean Ping alijitangaza mwenyewe kuwa rais na
kutoa wito kura kurudiwa kuhesabiwa kwa kura ambazo zilithibitisha kwamba Ali
Bongo ameshinda.
Hata
hivyo dunia nzima alijua kwamba Ping ndiye alikuwa rais wa nchi hiyo
Kizza Besigye
Kizza Besigye |
Nchini
Uganda Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye, ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa
Rais Yoweri Museveni, kupitia kanda ya video alionekana akifanya sherehe za
kula kiapo kuwa Rais wa Uganda baada yake kushindwa uchaguzini mwaka 2016 na Bw
Museveni.
Alikamatwa
na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
Bw
Besigye amekuwa akikamatwa na kushtakiwa mara kwa mara nchini humo.
Cahnzo:bbc Swahili
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments