WIZARA YATOA TAMKO KWA WALIOPOTEZA VYETI VYAO VYA ELIMU
Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia imewataka watanzania wote nchini waliopoteza vyeti vyao vya elimu watoe taarifa mapema katika sehemu husika na wasisubiri mpaka pale wanapokuwa na uhitaji navyo ndio waanze kuhangaika.
Mhe.William Ole Nasha |
Hayo
yameelezwa leo Bungeni na Naibu Waziri Wizara ya hiyo Mhe.William Ole
Nasha kwa niaba ya Waziri ya Waziri Sayansi,Teknolojia wakati alipokuwa anajibu
swali lililoulizwa na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato David Chumi.
Chumi alitaka kufahamu serikali ya
Tanzania kupitia Wizara ya Elimu ina mpango gani wa kuwasaidia watanzania
waliopoteza vyeti vyao vya elimu na kuvipata vingine.
Kwa upande
mwingine,Mhe.William Ole Nasha amesema muombaji wa cheti mbadala au uthibitisho
wa matokeo hupatiwa huduma baada ya kumaliza utaratibu wote uliyowekwa na
Wizara hiyo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments