WAUAWA KWA KUKATWA MAPANGA KWA MADAI YA USHIRIKINA


Watu watatu wameuawa katika matukio tofauti likiwamo la wanawake wawili kuuawa kwa kukatwa mapanga kutokana na imani za kishirikina katika kitongoji cha  Kilombero Wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Kamanda wa polisi Mkoani Rukwa George Kyando aliwataja waliouawa kuwa ni Salome Kisinza(50) na Rahel Pawa(22) walikatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na watu wasiojulikana.
Kyando alisema waliofanya mauaji hayo waliwavizia wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao ambapo walivunja mlango na kuingia ndani na kuanza kuwakata mapanga.
Alisema walimuua Salome na kumjeruhi Rahel baadaye walitoweka huku wakimwacha katika hali mbaya na alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa hospitali.
Kamanda Kyando alisema chanzo cha mauaji hayo inasadikiwa ni tuhuma za imani za ushirikina kwa kuwa Salome alikuwa akituhumiwa kumroga mume wake Jilala Mponeja ambaye amekuwa akiumwa kwa muda mrefu na anatibiwa kwa mganga wa jadi wilayani Kalambo mkoani humo.
Katika tukio jingine lililotokea saa tatu usiku katika Sekondari ya Tawheed Manispaa ya Sumbawanga mtu aliyefahamika kwa jina moja la Hassan (27) mkazi wa Kizwite aliuawa kwa kipigo akituhumiwa kwa wizi.
Alisema Hassan alikuwa anatuhumiwa kuiba bomba moja la chuma na misumari kilo moja na nusu,ambavyo thamani yake haijajulikana.
Alisema watuhumiwa wa mauaji hayo alimfungia Hassan ndani ya stoo kisha kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi alipofariki dunia.
Kamanda Kyando alisema watuhumiwa sita wa mauaji hayo akiwamo mlinzi wa stoo,mwalimu wa Sekondari ya Tawheed na wanafunzi wanne wanashikiliwa kwa mahojiano na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
Mwezi Desemba mwaka jana Mkuu wa jeshi nchini IGP Simon Sirro akiwa ziarani Mkoani Rukwa akitokea Mkoani Katavi alisema lazima mauaji yanayohusisha ushirikina yakomeshwe kwa kuwachukulia hatua watu wote wanaohusika huku Mkuu wa Mkoa huo Joachim Wangabo kwa nyakati tofauti akiomba ushirikiano baina ya viongozi wa dini na serikali ili kukomesha matukio hayo.
Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA