MBUNGE ALIYESIMAMIA KIAPO CHA RAILA ODINGA AKAMATWA
Mbunge wa Ruaraka Tom J Kajwang’ ambaye jana Jumanne alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga kwenye viwanja vya Uhuru Park Jumanne amekamatwa.
Mbunge
huyo amekamatwa leo mchana na maofisa wa polisi ambao hawakuwa wamevalia sare
nje ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi.
Alikamatwa
muda mfupi baada ya kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga
kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara
yao na posho.
Kajwang’
na mwanasheria mwingine Miguna Miguna,ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa matukio
katika viwanja vya Uhuru Park yaliyomalizikia kwa “kuapishwa” Odinga kama ‘rais
wa wananchi’.
Wakati
wa sherehe za kiapo Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi na alishangiliwa sana
na wafuasi wa Nasa.
Odinga
alikula “kiapo” huku Kajwang’ akiwa amesimama nyuma yake japokuwa wajibu wake
katika tukio hilo bado haujafahamika.
Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED
Comments