RAIS MAGUFULI ATOA AGIZO ZITO KWA KAMISHINA WA UHAMIAJI NCHINI
Rais John Magufuli ameitaka Idara ya Uhamiaji
kuhakikisha inapambana na wahamiaji haramu pasipo kumwogopa mtu.
Amemwagiza Kamishna wa Uhamiaji,Dk Anna
Makakala kuwachukulia hatua kali watumishi wake watakaoshindwa kutekeleza
wajibu wao ipasavyo.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli |
Dk.Magufuli akizungumza leo akizindua hati ya
kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam,amesema utambuzi wa wananchi
wanaoishi bila vibali na wenye vibali vilivyoisha ni muhimu.
Amesema uhamiaji ina jukumu kubwa katika
kutekeleza hayo.
Amesema awali Uhamiaji iligubikwa na matatizo yakiwamo ya utoaji hovyo wa vibali vya uraia, hata kwa watu ambao walikuwa hawana sifa.
Amesema awali Uhamiaji iligubikwa na matatizo yakiwamo ya utoaji hovyo wa vibali vya uraia, hata kwa watu ambao walikuwa hawana sifa.
Dk Magufuli amesema hiyo ndiyo sababu
iliyofanya akamteua Dk Makakala kuwa Kamishna. "Wanawake ni waaminifu sana
na ameanza kutatua matatizo haya."
Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi huo ni Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Wengine ni marais wastaafu Amani Abeid Karume na Ali Hassan Mwinyi,Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Ali Iddi.

Pia viongozi wa Serikali,Bunge,Baraza la
Wawakilishi,wa dini,wanasiasa,na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments