WATU WASIOJULIKANA WAILIPUA NYUMBA YA KIONGOZI WA UPINZANI KWA BOMU

Kiongozi mwenza wa Raila Odinga katika umoja wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA),Kalonzo Musyoka nyumba yake usiku wa kuamkia leo imepigwa bomu na watu wasiojulikana katika eneo la Karen, jijini Nairobi nchini Kenya.
Taarifa kutoka kwa OCPD wa Karen, Cunnigham Suiyanka amethibitisha taarifa hizo leo Jumatano Januari 31, 2018 kuwa ni kweli bomu hilo limelipuka katika nyumba hiyo na hakuna hata mmoja aliyeripotiwa kujeruhiwa kwenye tukio hilo.
Hata hivyo, Kamanda Suiyanka amesema tayari jeshi la polisi limefika eneo la tukio kufanya uchunguzi ili kuwabaini watu hao waliyohusika na tukio hilo.
Hayo yamejiri ikiwa ni masaa machache tangu Kalonzo Musyoka kutotokea jana Januari 30, 2018 kwenye sherehe za kujiapisha kwa kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga kuwa Rais wa wananchi wa Kenya sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Uhuru jijini Nairobi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA