RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA MZEE MAJUTO HOSPITALI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli amemtembelea
muigizaji mkongwe,Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam
ambako amelazwa akitibiwa.
Akizungumza
mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio
mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania
huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara.
Pamoja
na hayo,Mzee Majuto aliendelea kwa kusema ;“sisi wazee tunafarijika sasa hivi,viwanda kila kona vimetapakaa na leo
amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa
uoga maana hataki masihara.
Kwa
upande mwingine, Mzee Majuto amesema sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa
na masihara kama Dkt.John Magufuli.
Chanzo:Bongo5.com
Habari zaidi niP5TANZANIA LIMITED
Comments