MAJAMBAZI WAUA,WAJERUHI NA KUPORA MALI MGODINI MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kwa rasasi sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kuvamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo katika mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo uliopo Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi. Pamoja na kuwataja majeruhi,kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Jaffari Gwiyama Kitambwa,amemtaja aliyefariki kuwa ni Kalister Kalyalya(21) mkazi wa kata ya machimboni Wilayani Mpanda aliyepigwa risasi mgongoni na kutokezea tumboni.