MAJAMBAZI WAUA,WAJERUHI NA KUPORA MALI MGODINI MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watatu
kujeruhiwa kwa rasasi sehemu mbalimbali
za miili yao baada ya kuvamiwa na majambazi
usiku wa kuamkia leo katika mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo uliopo
Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.
Pamoja na kuwataja majeruhi,kaimu
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda Dkt.Jaffari Gwiyama Kitambwa,amemtaja
aliyefariki kuwa ni Kalister Kalyalya(21) mkazi wa kata ya machimboni Wilayani Mpanda aliyepigwa risasi
mgongoni na kutokezea tumboni.
Dkt.Kitambwa amewataja waliojerhiwa kuwa ni Joseph Panya Mahinja(39) mkazi wa mkoani Morogoro amevunjika mfupa wa bega,Mrisho Abdalla(41) makazi wa Kawajense alipigwa risasi kifuani upande wa juu na kutokezea begani upande wa kulia,Masunga Mwigulu mkazi wa Kasekese wilayani Tanganyika ambaye alipigwa risasi mkono wa kulia na kuvunjika mfupa wa mguu.
Dkt.Kitambwa amewataja waliojerhiwa kuwa ni Joseph Panya Mahinja(39) mkazi wa mkoani Morogoro amevunjika mfupa wa bega,Mrisho Abdalla(41) makazi wa Kawajense alipigwa risasi kifuani upande wa juu na kutokezea begani upande wa kulia,Masunga Mwigulu mkazi wa Kasekese wilayani Tanganyika ambaye alipigwa risasi mkono wa kulia na kuvunjika mfupa wa mguu.
Kwa upande Joseph Panya Mahinja(39)
mkazi wa mkoani Morogoro na Mrisho Abdalla makazi wa Kawajense Manispaa ya
Mpanda ambao walikuwa wakinunu dhabau hiyo,wamesema tukio la kuvamiwa kwao limetokea
jana usiku majira ya saa mbili usiku na limewaathiri kiafya.
Katika hatua nyingine Dkt.Kitambwa
amesema kuwa majeruhi wote wanatarajiwa kupelekwa hospitali ya taifa Muhimbili
kwa ajili ya matibabu zaidi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi huo
Bw.Amosi Kahega pamoja na mambo mengine amesema mgodi huo wenye wafanyakazi
zaidi ya 1000 umepatwa na athari kubwa ikiwemo kupoteza nguvu kazi ya taifa na
upotevu wa pesa na dhahabu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani
Katavi ACP Damasi Nyanda akithibitisha tukio hilo amesema jeshi la polisi
limeanza uchunguzi wa tukio hilo.
Hilo ni tukio la pili la linalohusisha
ujambazi Mkoani Katavi na kusababisha kifo ambapo mbali na tukio la Januari 22
mwaka huu lililohusisha mwanafunzi kuwawa na mtu anayesadikika kuwa ni
mwendesha bodaboda pia kuna tukio la Januari 27 mwaka huu katika kata ya Ugalla
ambapo Mtu mmoja aliuwawa na wengine zaidi ya watano kujeruhiwa baada ya
uvamizi wa watu wanatajwa kuwa ni mambazi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments