Posts

Showing posts from July 21, 2017

MKUU WA WILAYA YA MPANDA LILIAN MATINGA AMWAGIZA MKURUGENZI MTENDAJI MANISPAA YA MPANDA KUTAFUTA VIWANJA KWA AJILI YA WAKAZI WA MTAA WA MSASANI KABLA YA BOMOA BOMOA-Julai 21,207

Image
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Matinga,amemwangiza Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,kutafuta viwanja kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msaani kata ya Mpanda Hotel watakaobomolewa makazi yao kabla ya miezi sita waliyopewa kwisha. Katika picha kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda B.Lilian Charles Matinga(Picha na .Issack Gerald)

WAMILIKI VITUO VYA MAFUTA KATAVI,WAUNGA MKONO TAMKO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU MASHINE ZA KIELEKTRONIKS-Julai 21,2017

Image
BAADHI ya wamiliki wa vituo vya mafuta vilivyopo Mkoani Katavi wameunga mkono tamko la Rais linalowataka kufunga mashine zinazotoa risiti za kielekroniks Bw.Malick Saidi ambaye ni Meneja kwa kampuni ya Mafuta ya GBP,kwa upande wake amesema mfumo huo utawaokolea muda pamoja na kampuni yake kukusanya mapato yote kama inavyotakiwa. Aidha Bw.Saidi akatoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani Katavi kutokana na mfumo wa mashine za kielektroniks Wiki iliyopita,zaidi ya vituo vya mafuta 700 kote nchini vikiwemo vitano vilivyopo Mkoani Katavi vilifungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa madai ya kuikosesha serikali mapato kutokana na kutotumia mashine za kielektroniks EFD. Rais John Magufuli juzi akiwa Mkoani Kagera,ametoa siku 14 kwa makampuni ya mafuta nchini kuhakikisha wanafunga mashine hizo kinyume na hapo kampuni ambayo haitatekeleza agizo hilo Rais ameagiza ifungiwe na kunyang’anywa leseni ya Biashara. Muuzaji na mnunuzi wote wanajikuta hatiani kwa kukiuka ...

MKOA WA KATAVI WAFAULISHA MWANAFUNZI KATI YA KUMI BORA KITAIFA KIDATO CHA SITA 2017-Julai 21,2017

Image
JUMLA ya wanafunzi 574 kati ya 588 waliofanya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2017 mkoani Katavi wamefaulu huo ambapo Penina Mwalingo wa shule ya sekondari Mpanda Girls akishika nafasi ya 9 kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa waliofanya vizuri. Afisa Elimu wa Mkoa Katavi Mwalimu Godfrey Kalulu amesema Ufaulu kwa shule za Sekondari za kidato cha sita mkoani Katavi umeongezeka kwa asilimia 3.5 ambapo kwa mwaka 2017 ufaulu ni asilimia 69.5 ukitofautisha na asilimia 66.0 ya mwaka 2016. Katika picha ni Baadhi ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mpanda Ndogo(PICHA NA Issack Gerald) Kalulu amesema shule ya Sekondari Karema imeshika nafasi ya kwanza Mkoani Katavi huku kitaifa ikishika nafasi ya 50 kati ya 449.