WAMILIKI VITUO VYA MAFUTA KATAVI,WAUNGA MKONO TAMKO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU MASHINE ZA KIELEKTRONIKS-Julai 21,2017

BAADHI ya wamiliki wa vituo vya mafuta vilivyopo Mkoani Katavi wameunga mkono tamko la Rais linalowataka kufunga mashine zinazotoa risiti za kielekroniks

Bw.Malick Saidi ambaye ni Meneja kwa kampuni ya Mafuta ya GBP,kwa upande wake amesema mfumo huo utawaokolea muda pamoja na kampuni yake kukusanya mapato yote kama inavyotakiwa.

Aidha Bw.Saidi akatoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani Katavi kutokana na mfumo wa mashine za kielektroniks

Wiki iliyopita,zaidi ya vituo vya mafuta 700 kote nchini vikiwemo vitano vilivyopo Mkoani Katavi vilifungwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa madai ya kuikosesha serikali mapato kutokana na kutotumia mashine za kielektroniks EFD.

Rais John Magufuli juzi akiwa Mkoani Kagera,ametoa siku 14 kwa makampuni ya mafuta nchini kuhakikisha wanafunga mashine hizo kinyume na hapo kampuni ambayo haitatekeleza agizo hilo Rais ameagiza ifungiwe na kunyang’anywa leseni ya Biashara.

Muuzaji na mnunuzi wote wanajikuta hatiani kwa kukiuka kifungu cha sheria namba 38 ikiwa itathibitika kuwa hakuna risiti ya mashine ya kielektroniks iliyotolewa na faini yake kwa wahusika kwa mjibu wa sheria hiyo ni hadi shilingi milioni 4.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA