MKOA WA KATAVI WAFAULISHA MWANAFUNZI KATI YA KUMI BORA KITAIFA KIDATO CHA SITA 2017-Julai 21,2017

JUMLA ya wanafunzi 574 kati ya 588 waliofanya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2017 mkoani Katavi wamefaulu huo ambapo Penina Mwalingo wa shule ya sekondari Mpanda Girls akishika nafasi ya 9 kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa waliofanya vizuri.

Afisa Elimu wa Mkoa Katavi Mwalimu Godfrey Kalulu amesema Ufaulu kwa shule za Sekondari za kidato cha sita mkoani Katavi umeongezeka kwa asilimia 3.5 ambapo kwa mwaka 2017 ufaulu ni asilimia 69.5 ukitofautisha na asilimia 66.0 ya mwaka 2016.
Katika picha ni Baadhi ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mpanda Ndogo(PICHA NA Issack Gerald)
Kalulu amesema shule ya Sekondari Karema imeshika nafasi ya kwanza Mkoani Katavi huku kitaifa ikishika nafasi ya 50 kati ya 449.
Shule ya Sekondari,Usevya imeshika nafasi ya pili kimkoa huku kitaifa ikishika nafasi ya 239 kati ya 449 ambapo kwa upande Mpanda girls kitaifa imekuwa ya 278 kati 449 na kushika nafasi ya tatu kimkoa.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa Shule ya  Mpanda gils  Abdalah Dawa  na  Mkuu wa shule ya Usevya  Denice Tilia wamesema Mkoa wa Katavi unatakiwa kujipanga zaidi ili kufaulisha wanafunzi kwa kiwango kizuri kuliko sasa.
Mkoa wa Katavi umekuwa ukifanya vizuri kielimu kuanzia shule ya Msingi mpaka kidato cha sita ambapo Mkoa umekuwa ukishika nafasi ya kwanza hadi ya tatu.

Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA