MKUU WA WILAYA YA MPANDA LILIAN MATINGA AMWAGIZA MKURUGENZI MTENDAJI MANISPAA YA MPANDA KUTAFUTA VIWANJA KWA AJILI YA WAKAZI WA MTAA WA MSASANI KABLA YA BOMOA BOMOA-Julai 21,207
MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian
Matinga,amemwangiza Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,kutafuta
viwanja kwa ajili ya wakazi wa Mtaa wa Msaani kata ya Mpanda Hotel watakaobomolewa
makazi yao kabla ya miezi sita waliyopewa kwisha.
Katika picha kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda B.Lilian Charles Matinga(Picha na .Issack Gerald) |
Bi.Matinga ametoa agizo hilo leo
katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mpanda Hotel katika
viwanja vya shule ya Sekondari Kashaulili.
Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya amesema
serikali imezuia wakazi kufanya shughuli yoyote katika eneo la Jeshi la
Wananchi wa Tanzania lilipo Manispaa ya Mpanda.
Nao,wakazi wa mtaa wa Msasani wameomba
kupewa viwanja kwa bei nafuu kulingana na hali ngumu ya maisha waliyonayo kawa
sasa,ambapo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bw.Leonard Kilamhama pamoja
na mambo mengine,amesema manispaa ya Mpanda italifanyia kazi haraka suala la
wakazi wa mtaa wa msasani kabla ya hatua ya bomoabomoa itakalosababisha zaidi
ya nyumba 200 kubomolewa mwezi Januari mwakani.
Shirika la reli Tanzania TRL,wiki
iliyopita lilitoa tamko kuwa hakuna mkazi yeyote atakayebaki akiendelea kuishi
katika eneo la hifadhi ya reli ambapo hata hivyo utata ambao bado upo ni mita
ngapi ambapo kwa sasa zinatajwa mita 30,75 na 215 ambapo mita halali
hazijajulikana.
Habarika zaidi P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments