UKAWA WAMPITISHA RASMI LOWASSA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA
Edward Lowassa Mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa NA MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM Chama cha demokrasia na maendeleo chadema leo kimemuidhinisha Edward lowasa kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Wajumbe wa mkutano mkuu wa chadema uliofanyika leo Jijini Dar Es salaam wamepiga kura ya kuridhia kiongozi huyo aliyejiunga na upinzani akitokea chama tawala CCM kuwa mgombea Kiti hicho cha urais Kupitia chama hicho. Mwanasiasa huyo Mkongwe hapa Nchini amekuwa akiyagawa maoni ya Watanzania tangu akihame chama cha Mapinduzi na Kuhamia chama cha chadema tang u vikao vya uteuzi vya ccm kumpitisha mgombea wa urais kulikata jina lake. Hata hivyo katibu mkuu wa chadema Wilbroad Slaa hakuhudhuria mkutano huo mkuu Kutokana na kuwepo kwa taarifa kuwa hakufurahishwa na uamuzi wa chadema kumpo...