WENYE SIFA YA KUPIGA KURA KATAVI WATAKIWA KUHAKIKI MAJINA YAO KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA



Nembo ya tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania

Na.Tume ya taifa ya Uchaguzi-KATAVI
WANANCHI  Mkoani Katavi wametakiwa Kufika katika Vituo vyao walivyojiandikishia  Katika daftari la Mpiga Kura ili kuhakiki taarifa zao  Katika daftari la hilo.

Kwa Mjibu wa Tangazo lililotolewa na Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC Zoezi hilo limeanza Augost Mosi mwaka huu ili kutoa fursa kwa wananchi waliojiandiksha Kuhakiki taarifa zao zilizokosewa kabla ya Muda wa Kupiga Kura.
Jaji mstaafu Damian Lubuva mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzio Tanzania

Pamoja na Mkoa wa Katavi Mikoa mingine inayotakiwa kuanza zoezi hilo ni Rukwa,Njombe,Iringa,Mtwara,Lindi,Dodoma,Singida,Tabora na Kigoma.


WASIFU WA   DAMINANI LUBUVA - Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Damian Zefrin Lubuva alizaliwa tarehe 21 Septemba 1940 katika kijiji cha Haubi Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma.
Elimu
Alipata Elimu ya Msingi katika shule ya Kuta kuanzia mwaka 1949 hadi 1952 na katika shule ya kati ya St. Gabriel Catholic Kondoa kuanzia mwaka 1953 hadi 1956. Baadaye katika shule ya Sekondari ya St. Francis (Pugu) mwaka 1957 hadi 1962 ambapo alisoma Kidato cha Kwanza hadi cha Sita. Mwaka 1963 alijiunga na Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki ambacho sasa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alihitimu Shahada ya Kwanza ya Sheria mwaka 1966.
Kazi
Tarehe 5 Aprili, 1966 aliajiriwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa Wakili wa Serikali. Mwaka 1968 alihamishwa kwa muda (seconded) kuwa Mwanasheria wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi hadi 1969. Kati ya mwaka 1969 hadi 1972 alifanya kazi kama Wakili wa Serikali Mfawidhi katika kanda ya Arusha na baadaye aliteuliwa kuwa Wakili wa Serikali Mkuu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mwaka 1975 hadi 1976 alikuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Sheria Tanzania (Tanzania Legal Corporation). Mwaka 1976 aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kazi aliyoendelea nayo hadi mwaka 1977.
Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kazi aliyoifanya hadi mwaka 1983. Kati ya mwaka 1984 na 1985 alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria. Tarehe 5 Novemba 1985 aliteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali hadi mwaka 1993 alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania hadi alipostaafu Utumishi wa umma mwaka 2008. Kati ya mwaka 2009 na 2011 alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Sekreterieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Tarehe 19 Disemba 2011 hadi sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Nyadhifa nyingine
Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Umoja wa Tume za Uchaguzi katika nchi za SADC . Kuanzia Mwaka 2012 hadi 2014
Mjumbe wa Tume ya Mahakama (Judicial Service Commission of Tanzania). Kuanzia 2005 – hadi 21 Septemba, 2008:

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA