VIONGOZI WA UMMA TANZANIA WATAKIWA KUWA WAZALENDO KUPITIA WANAOWAONGOZA
Na.Issack Gerald-KATAVI
Viongozi wa umma hapa nchini
wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Uzalendokatika kutekeleza mahitaji ya
wanaowaongozana siyo kwa maslahi binafsi.
Wito huo umetolewa leo na wajumbe wa
semina ya utawala bora wa rasilimali asilia inayofanyika katika manispaa ya
Mpanda.
Wamesema kuwa miradi mingi ya
maendeleo imekuwa haitekelezeki kwa wakati katika maeneo mengi hapa nchini,
kutokana na watawala kutoa kipaumbele katika masuala binafsi kwa kutumia
rasimaliza taifa na kusahau kuwapa wananchi mahitaji ya msingi.
Semina hiyo inayofanyika kwa
usimamizi wa taasisi ya Jane Goodall inayojishughulisha na uhifadhi wa
mazingira, na kuhudhuriwa na wadau wa mazingira kutoka wilaya za Mpanda,
Nsimbo, Uvinza na Kigoma, inatarajiwa kukamilika ijumaa wiki hii.
Comments