MBUNGE JIMBO LA NKASI KUSINI ATAKA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA JIMBONI KWAKE,SERIKALI YAMJIBU
Na.Issack Gerald-Dodoma kuhusu (Rukwa) SERIKALI imesema mwaka wa fedha 2015/2016 ilitenga Shillingi million 300 kwa ajili matengenezo na ujenzi wa Barabara ya Kitosi- Wampembe katika Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ili kufanya Barabara hiyo iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.