WAWILI WAJERUHIWA,YUMO MAMA ALIYEJERUHIWA KWA KUCOMWA KISU KWENYE TITI.
Na.Issack
Gerald-Mpanda
Mtu
mmoja aliyejulikana kwa jina la Zuhura Salum(34), mkazi wa Majengo alijeruliwa
kwa kuchomwa na kisu kwenye titi la kulia na Iddy Saleh(24), mkazi wa majengo
na kumsababishia maumivu makali.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo
tarehe 29.01.2016 majira ya saa tatu asubuhi katika maeneo ya Majengo “B” Kata
na Tarafa ya Kashaulili Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
Kamanda
Kidavashari amesema kuwa mhanga na mtuhumiwa walikuwa wamelala kwenye nyumba ya
kulala wageni inayojulikana kwa jina la maridadi ndipo mtuhumiwa aliamka na
kumvizi akiwa usingizini na kumchoma na kisu kwenye titi la kulia.
Chanzo
cha tukio hili bado kujulikana ambapo hata hivyo mtuhumiwa anashikiliwa na
Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakmani kujibu
tuhuma inayomkabili.
Wakati
huo huo katika tukio lingine mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Kalekwa
Otto(28), mkazi wa kamukuswe alijeruliwa kwa kukatwa na panga mkono wa kulia na
kwa kushoto na Manyara Otto na kumsababishia majeraha
Aidha
Kamanda Kidavashari amesema kuwa tukio hili limetokea juzi 01.02.2016 majira ya
saa moja kijiji cha kamkuswe kata na
tarafa ya mwese wilayani mpanda mkoani katavi.
Amesema
kuwa mtuhumiwa na mhanga ni mtu na kaka yake ambapo Siku ya tukio wakiwa kwenye
kilabu cha pombe huku wakiendelea kunywa ndipo ulipozuka ugomvi kati ya ndugu
hawa wawili na Manyara Otto alipomkata kwa panga na mara baada ya kutenda kosa
hilo alitokomea kusikojulikana.
Hata
hivyo Chanzo cha tukio hili ni ugomvi wa kifamilia kati ya ndugu hawa wawili na
Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka alipokimbilia mtuhumiwa ili kujibu tuhuma
inayomkabili.
Wakati
huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi amewataka wananchi kujenga mazoea ya
kuwasilisha matatizo yao katika mamlaka za kisheria ili yaweze kupatiwa ufumbuzi
na badala yake waachane na tabia ya kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya
vitendo viovu vinavyopelekea matatizo makubwa ndani ya familia.
Comments