MBUNGE JIMBO LA MPANDA MJINI ATAKA UJENZI CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA KATAVI UKAMILIKE
Na.Issack Gerald-Dodoma
Mbunge wa Mpanda Mjini Mheshimiwa
Sebastian Kapufi ameiomba Serikali kuweka nguvu yake katika ujenzi wa chuo
kikuu cha kilimo kinachotarajiwa Mjini Mpanda kwa ajiri ya Kuongeza ajira kwa
wakazi wa Mkoa wa Katavi na Mioko mingine.
Bungeni Dodoma |
Mbunge wa Mpanda Mjini Mheshimiwa Sebastian Kapufi akiwa na watoto katika Familia yake kabla ya kwenda bungeni wiki iliyopita |
Mheshimiwa Sebastian Kapufi ameuliza
swali hilo akiwa bungeni Mjini Dodoma ambapoa akijibu swali hilo,Naibu waziri
wa Elimu, sayansi,teknolojia na ufundi Injinia Stela Martin Manyanya
amesemakuwa tayari tume ya vyuo viku ilikwishatoa hati kwa ajiri ya ujenzi wa
chuo kikuu hicho kinachomilikiwa na Manispaa
ya Mpanda ambapo amesemakuwa serikali itaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu
nakiufundi ili kukamilisha ujenzi wa Chuo kikuu cha kilimo cha Katavi.
Aidha Serikali kupitia wizara ya Elimu,
sayansi,teknolojia na ufundi imeshauri Manispaaya Mpanda kushirikisha balaza la
madiwani ili kuondoa hali ya sintofahamu juu ya ujenzi wa chuo hicho ambacho
kama kingekuwa kinaendelea kujengwa mpaka sasa kingekuwa kimekwishapata Doala
za kimarekani Milioni 2.5 kwa udhamini wa benki ya biashara ya AFRICAN TRADING
INSURANCE AGENCE.
Hata hivyo Injini Stela Manyanya
amesema Manispaa ilikwishapata eneo la ekari 500 kwa ajiri ya ujenzi wa ujenzi
wa chuo hicho.
Kwa upande wake Waziri wa elimu sayansi,teknolojia
na ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa chuo hiki kinajengwa na
Manispaa baada ya kuomba wizarani juu ya ujenzi wa chio hicho.
Uamuzi wa Ujenzi wa Chuo kikuu cha
Kilimo ulitolewa mwaka feb 11,2011 kupitia vikao vya kisheria vya Halmshauri ya
Manispaa ya Mpanda kwa kuzingatia sheria ya seriklai za mitaa serikali ya mtaa
no.8 ya 1982(5) kifungu 53 na 54 1(a) na
(b) na 2 (b) na (c).
Tume ya vyuo vikuu ilitoa hati ya
usajiri wa awali ya uanzishwaji wa chuo hiki kwa barua yenye kumbukumbu no.TCU/A/40/1A/V34
YA 31/01/2012 ambapo Manispaa ya Mpanda ilikuwa kikishirikiana wadau mbalimbali
kikiwemo chuo cha kilimo cha Uingereza kukamilisha masharti ya uanzishwaji wa
chuo hiki.
Comments