ZAIDI YA BILIONI 26 NA BILIONI 43 ZAIDHINISHWA NA BALAZA LA MADIWANI NSIMBO KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MWAKA WA FEDHA 2016/2017
Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Nsimbo
Mkoani Katavi imeidhinisha kiasi cha shilingi billion 26,043,182,000 (Bilioni 26 milioni 43 na mia moja themanini
na mbili elfu) kwa ajili ya kutekeleza
MIRADI mbalimbali iliyopangwa kufanyika katika Halmashauri hiyo kwa mwaka wa
fedha 2016/2017.
Fedha hizo zimeidhinishwa na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Nsimbo katika kikao cha bajeti ya mwaka wa fedha 206-2017 kilichofanyika leo
katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Akisoma Bajeti hiyo mkuu wa idara ya
mipango takwimu na ufuatiliaji Fredinand Filimbi amesema bajeti iliyotengwa
imeandaliwa kwa imezingatia sera na
miongozo mbalimbali ya kitaifa.
Aidha bw. Filimbi amefafanua
mchanganuo wa fedha hizo utatumika katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na
mishahara,miradi ya maendeleo, na matumizi ya kawaida.
Amesema kiwango cha mapato ya ndani
kwa mwaka wa fedha 2016-2017 kimeongezeka kwa asilimia 12 na kutaja baadhi ya vyanzo
vya ukusanyaji wa mapato hayo ikiwemo ushuru wa mifugo,magulio,nyama na vyombo
vya uvuvi.
Aidha akifunga kikao hicho Mwenyekiti
wa baraza la madiwani Rafael Kalinga ambaye ni diwani wa kata ya Machimboni amewataka
madiwani na watumishi kuendelea kushirikiana ili kufikia malengo ya bajeti hiyo
pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato ,pia amewataka wakuu wa idara kuhakikisha wanatekeleza miradi ya nyuma
ambayo ilitengewa fedha.
Comments