MAKAMU WA RAIS AFUNGIWA MAISHA
Makamu wa Rais wa shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Michael Wambura amefungiwa kifungo cha maisha cha kutojihusisha na mchezo wa soka popote pale. Michael Wambura Jana mchana afisa habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo aliwaambia waandishi wa habari kuwa Wambura amefanya makosa hayo huku akijua anashusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na katiba ya TFF. Ndimbo alisema Wambura alikuwa na uhuru wa kufika mwenyewe mbele ya kamati na kutoa utetezi wake kwa njia mdomo,kutuma kwa maandishi au kupeleka mashahidi au kutuma mwakilishi ambaye ataambatana na barua ya uwakilishi ambapo Wambura alituma mwakilishi ambaye ni Wakili Emanuel Muga kwa ajili ya kumtetea. Alisema kamati hiyo iliyokaa jana ikiongozwa na Mwenyekiti wake Hamidu Ally Mbwezereni,wamemkuta na makosa matatu yatakayomfanya Wambura asijihusishe na masuala ya soka. Kosa la kwanza amevunja kifungu no 73 kwa kupokea malipo yasiyo halali ya TFF, ambapo faini yake ni milioni 10, kutojihusisha na sok...