MAKAMU WA RAIS AFUNGIWA MAISHA
Makamu wa Rais wa shirikisho la mpira
wa Miguu Tanzania (TFF),Michael Wambura amefungiwa kifungo cha maisha cha
kutojihusisha na mchezo wa soka popote pale.
Michael Wambura |
Jana mchana afisa habari wa TFF
Clifford Mario Ndimbo aliwaambia waandishi wa habari kuwa Wambura amefanya
makosa hayo huku akijua anashusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na
katiba ya TFF.
Ndimbo alisema Wambura alikuwa na uhuru wa kufika mwenyewe
mbele ya kamati na kutoa utetezi wake kwa njia mdomo,kutuma kwa maandishi au
kupeleka mashahidi au kutuma mwakilishi ambaye ataambatana na barua ya
uwakilishi ambapo Wambura alituma mwakilishi ambaye ni Wakili Emanuel Muga kwa
ajili ya kumtetea.
Alisema kamati hiyo iliyokaa jana ikiongozwa
na Mwenyekiti wake Hamidu Ally Mbwezereni,wamemkuta na makosa matatu
yatakayomfanya Wambura asijihusishe na masuala ya soka.
Kosa la kwanza amevunja kifungu no 73
kwa kupokea malipo yasiyo halali ya TFF, ambapo faini yake ni milioni 10,
kutojihusisha na soka miaka mitano au maisha.
Kosa la pili kugushi malipo kwa jina
la TFF enzi hizo (FAT), ambapo amezuiliwa kujihusisha na soka kwa miaka 5.
Kosa la tatu linalomkabili ni
kushusha hadhi ya TFF,kosa ambalo adhabu yake iliyotolewa ni kutojihusisha na soka
maisha.
Kwa upande mwingine,Kamati ya Maadili
ya TFF imesema adhabu hiyo iliyotolewa dhidi ya Michael Wambura imezingatia
vigezo na masharti.
Hata hivyo,wakili wake Emmanuel Muga
amesema,hakupewa nafasi ya kumtetea mteja wake kwa sababu kamati ilikuwa na
dhamira yake ya kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo (jana Machi 14,
2018).
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments