RAIS MAGUFULI AAGIZA WAFANYABIASHARA WADOGO WA STENDI MOROGORO WASIBUGHUDHIWE
Mwanamke aliyejitambulisha kwa
jina moja la Avintishi,leo amejitoa
kimasomaso na kumueleza Rais John Magufuli kuhusu kero wanayopata
wafanyabiashara ndogondogo ikiwamo kunyang’anywa bidhaa zao.
Mwanamke huyo ametoa kero hiyo leo,katika
uzinduzi wa kiwanda cha Sigara cha Philip Morris mkoani Morogoro.
Baada ya kueleza hayo,Rais alimuita
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro,John Mugarula kujibu kero
zilizoibuliwa na mama huyo ambapo Mkurugenzi huyo, alisema wanawaondoa
wafanyabiashara hao kwa sababu wametengewa maeneo maalumu huku akisema sababu ya
suala la kipindupindu.
Baada ya hapo Rais,alimuhoji mama
huyo,ni kiasi gani alitozwa na askari mgambo wa manispaa,mama huyo akaeleza
kuwa alitozwa Shilingi 200, 000.
Rais alihoji tena,iwapo mama huyo
anamkumbuka askari mgambo aliyemtoza kiasi hicho? Ambapo Baada ya kusema hayo,Rais
alimpa mama huyo fedha na kumtaka mkurugenzi kumpa kiasi kingine cha fedha mama
huyo.
Kufuatia hatua hiyo,Rais aliagiza
kuanzia leo,wafanyabiashara hao wasibughudhiwe kwa sababu ni watoto wa maskini.
Wageni wengine waliokuwapo katika
uzinduzi huo ni Mbunge wa Viti Maalumu,(CCM) Getrude Rwakatare ambaye ni
miongoni mwa waliomchangia mwanamke huyo fedha.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments