MWANAFUNZI AFARIKI MAZINGIRA YA KUTATANISHA POLISI WAWASHA TAA NYEKUNDU
Jeshi
la polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa wawili kufuatia kifo cha
kutatanisha cha mwanafunzi wa kike wa kidato cha sita Sundi George.
Kwa
mjibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Juma Bwire amesema mwanafunz huyo alikuwa
akisoma katika shule ya sekondari Mwembetogwa.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda Bwire amesema mnamo Machi 12 mwaka
huu mwanafunzi huyo akiwa na sare za shule alitoka nyumbani kwao kuelekea
shuleni lakini hakurudi hadi mwili wake ulipopatikana maeneo hayo.
Kamanda
Bwire amesema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mwanafunzi
huyo.
Hata
hiyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa mtu yoyote anayehusika katika
tukio hilo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments