ACT-WAZALENDO WALAANI UHARIFU MKOANI KATAVI
Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo
Mkoani Katavi, wamelaani matukio mbalimbali ya uharifu yanayoendelea kujitokeza
Mkoani Katavi na kusababisha mauaji ya raia na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo John
Malack pamoja na katibu wa chama hicho Bw.Joseph Mona wamevishauri vyombo vyote
vya ulinzi na usalama kutafuta namna ya kudhibiti waharifu ili kuimarisha usalama
wa raia ma mali zao.
Kwa upande wao baadhi ya vijana
Mkoani Katavi wamesema, ukosefu wa ajira kwa vijana wengi waliopo mitaani ni
miongoni mwa vyanzo vinavyochangia kuongezeka kwa uharifu.
Kuanzia mwezi Januari mpaka Machi
mwaka huu,zaidi ya watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti
yakiwemo matukio mawili ya ujambazi Januari 27 kata ya Ugalla,Februari 25 mwaka
huu katika Mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo wilayani Mpanda na lingine la
Januari 22 likihusisha kifo cha mwanafunzi aliyeuwawa kikatiri wilayani
Tanganyika.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments