RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI WAPYA NGAZI YA WIZARA NA MIKOA,ABADILISHA WAKUU WA MIKOA GHAFLA
Na.Issack Gerald-Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Wakuu wapya,Naibu Makatibu Wakuu wapya na Wakuu wa Mikoa wapya sita. Rais Mgaufuli mara baada ya kuwaapisha walioteuliwa ,amewaagiza walioapishwa kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati bila kusubiri kusukumwa. Katika hatua nyingine,rais Magufuli amefanya mabadiliko ya ghafla akiwa ikulu wakati akiwaapisha walioteuliwa,ambapo Bi. Christine Solomon Mndeme aliyetakiwa kuwa mkuu wa Dodoma atakuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma. Aidha aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge,ameteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma akichukua nafasi ya Christine Solomon Mndeme aliyetakiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Wakati huo huo Rais Magufuli amesema shilingi bilioni 147 alizoidhinisha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu,zitolewe kama inavyotakiwa kwa wakati na pia kwa wanafunzi wenye sifa. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au u...