RC KATAVI:UJENZI WA ZAHANATI YA KAKESE UKAMILIKE KABLA YA DESEMBA MOSI MWAKA HUU

Na.Issack Gerald-Katavi
MKUU wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya muhuga,ameagiza ujenzi wa wadi ya wazazi katika zahanati ya kata ya Kakese kukamilika kabla ya Desemba Mosi mwaka huu.

Muhuga ametoa agizo hilo leo wakati akifanya ukaguzi wa maendeleo ya zahanati hiyo
Kwa upande wake  kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bi.Mary Lihululaamesema tayari wameshapokea shilingi milioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo na Shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya ukarabati wa wa jingo la zahanati.
Zahanati ya Kakese inahudumia vijiji vya Mbugani na mkwajuni vijiji ambavyo vinaaminika kuwa na wakazi wengi kutokana na kuwa na watu wengi wanaojishghulisha na kilimo cha mazao kama mpunga na mahindi.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA