WALIMU WANAUSUBIRI MWEZI NOVEMBA KWA HAMU, MADARAJA, MISHAHARA NA MENGINE KEDEKEDE
Na.Issack Gerald-Nsimbo
SERIKALI inatarajia kuanza kulipa
madeni,kuajiri na kupandisha madaraja kwa walimu kuanzia mwishoni mwa mwezi
Novemba mwaka huu.
Hatua hiyo imethibitishwa na Mjumbe wa kamati
utendaji ya taifa ya chama cha walimu Tanzania CWT Costantine Maricery,ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo katika
halashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Awali katibu wa chama cha walimu Tanzania CWT
Halashauri ya Wilaya ya Nsimbo,Dunstan Mshanga katika risala yake
amesema,pamoja na walimu kuidai serikali zaidi ya shilingi milioni 435,pia
wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vitendea kazi suala ambalo mgeni rasmi
amesema yanafanyiwa kazi.
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti wa chama cha walimu Tanzania CWT Mkoani Katavi Mwl
John Gerigori Mshota mbali na kuwataka walimu kuwa na nidhamu mahala pa kazi
amesema chama hakitakubaliana na mwajiri atakayemlazimisha mwalimu kufanya kazi
nje ya muda unaojulikana kisheria.
Nao baadhi
ya walimu wanachama CWT katika Halmashauri ya Nsimbo,wamesema mkutano mkuu
umejibu ipasavyo haki za walimu kama inavyotakiwa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments